Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli leo hii Mei 5, 2018 amezindua daraja la mto Kilombero ambalo limepewa jina la Magufuli, daraja hilo lina urefu wa mita 384 linalounganisha Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero ambapo ujenzi wa daraja hilo umegharimu kiasi cha fedha Shilingi Bilioni 61.223 za Kitanzania zilizotolewa na Serikali ya Magufuli.

Katika uzinduzi huo Rais JPM amehoji kwa nini wameliita Daraja la Magufuli, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ametoa jina hilo kutokana na juhudi alizozifanya Rais Magufuli wakati akiwa waziri wa ujenzi.

”Mheshimiwa Rais kwa mamlaka niliyopewa natangaza daraja hili litaitwa Magufuli hii ni kutokana na juhudi kubwa uliyoiweka katika kufanikisha ujenzi wa daraja hili” amesema Mbarawa.

Bonyeza kitufe hapa chini kutazama video hiyo.

Video: Rayvany aiachia ngoma yake mpya 'Pochi nene'
Kisiwa cha Hawaii chakumbwa na mlipuko wa Volkano na kimbunga