Diamond Platinumz mapema leo hii ameachia ngoma yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Baila’ ngoma ambayo ipo kwenye albamu yake ya A boy From Tandale iliyoachiwa rasmi mnamo Machi 16, 2018 ikiwa ni wimbo wake wa tisa kwenye albamu hiyo.

Amefanya ngoma hiyo akiwa amemshirikisha msanii toka Marekani ambaye pia ni mshindi wa Tuzo za Grammy, Miri Ben-Ari, huyu jamaa ni mzaliwa wa Israel lakini ni moja ya wasanii wakubwa nchini Marekani kutokana na kazi zake ambazo amefanya na wasanii wakubwa nchini humo akiwemo, Kanye West, Jay Z, Alicia Keys, Jane Jackson, Tarkan na Armin Van Buuren pamoja na wengine.

Baila ni neno la kispanish likimaanisha kucheza, na tayari ngoma hii inaongoza kutazamwa katika chati za Video YouTube, kama bado hujaitazama ngoma ya ‘Baila’ Dar24 imekuwekea hapa

Itazame.

TBS, TFDA wafunguka tishio la sukari feki
Mlipuko wa tenki la kemikali wajeruhi, Jeshi lanena