Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) limesema kuwa litaendelea kusimamia sekta ya madini katika kutoa utaalamu kwa wachimbaji wadogo wadogo katika kuhakikisha wanakua ikiwa ni pamoja kuongeza Pato la Taifa.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenziwa shirika hilo, Alex Rutagwelela alipokuwa akizungumza na Dar24 Media katika Mkutano wa wadau wa sekta ya Madini ambapo amesema kuwa Stamico iko wazi katika kuhudumia wachimbaji wa Madini wadogo masaa 24.
 
Amesema kuwa kwasasa wana mtambo wa uchorongaji mpya na wa kisasa, hivyo amewataka wachimbaji wadogo wadogo kuchangamkia fursa kwa kutumia gharama nafuu katika shughuli zao za uchimbaji.
 
“Wachimbaji wa madini wadogo watumie shirika lao katika ushauri ili kuweza kuchimba kisasa, waachane na kuchimba kimazoea wa bila mafanikio” amesema Rutagwelela.
 
Aidha, Rutagwelela amesema kuwa mkutano wa Madini ulikuwa na maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi hivyo kazi yao ni kutekeleza maagizo ili sekta ya madini iwe nguzo ya uchumi kutokana na rasilimali zilizopo ziendelezwe kwa maendeleo.

Kizimbani kwa kuchapisha uongo dhidi ya Rais Magufuli
Shil. Mil. 3 zamsweka ndani mwenyekiti wa AMCOS

Comments

comments