Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Ujerumani imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la mabara mara baada ya kuitandika timu ya Taifa ya Mexico magoli manne kwa moja.

Aidha, katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua uliokutanisha miamba hao wa soka duniani, alikuwa ni mchezaji wa Ujerumani, Leon Goretzka alifungua kalamu ya magoli baada ya dakika ya 6 ya mchezo huo kufunga goli huku dakika mbili baadaye dakika ya 8 akipachika la pili.

Magoli mengine ya Ujerumani yaliwekwa kambani na Timo Warner dakika ya 59 huku Amin Younes akikomelea msumari wa mwisho katika dakika ya 90.

Bao pekee na la kufutia machozi la Mexico lilipachikwa kimiani na Marco Fabian dakika ya 89, ambapo kwa sasa timu ya Ujerumani itakwaana na Chile katika fainali itakayopigwa siku ya jumapili.

Video: Pigo zito TFF, Simba, Miswada ya 'ncha kali' yatua bungeni
Magazeti ya Tanzania leo Juni 30, 2017