Msemaji wa Rais wa Ufilipino, Harry Roque amesema kuwa Mahakama ya Kimataifa ya makosa Jinai imeanza kuchunguza tuhuma za vitendo vya jinai dhidi ya binadamu zilizoelekezwa kwa rais huyo.

Roque amesema kuwa Mahakama hiyo iliyopo The Hague imemjulisha Rais Rodrigo Duterte kwamba imefungua uchunguzi wa awali juu ya malalamiko yaliyofunguliwa mwaka 2017.

Aidha, Malalamiko hayo yalifunguliwa na wakili mmoja wa Ufilipino kufuatia ukamataji wa kinyama katika vita dhidi ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa jumla ya watu 4,000 wameuwawa tangu kuingia madarakani kwa Duterte mwaka 2016.

Pia Wanaharakati wa kupigania haki za bindamu wamesema kuwa ahadi ya Duterte ya kuwauwa maelfu ya wanaojishughulisha na madawa ya kulevya imepelekea polisi kufanya mauaji yaliyovuka mpaka dhidi ya wanaoshukiwa kuwa ni watumiaji na wafanya biashara wa madawa hizo.

Hata hivyo polisi wamekanusha tuhuma hizo za mauaji na wanasisitiza kuwa wamekuwa wakiwauwa washukiwa ambao walikuwa na silaha kwa kujihami wakati wa operesheni halali ya kupambana na madawa ya kulevya.

 

Mhubiri matatani kwa kudai wanawake ni chanzo cha uovu
Video: Wauza dawa za kulevya wawekwa kikaangoni