Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ametangaza vita na waalimu wa kiume katika wilaya yake na kusema kuwa ameanzisha oparesheni ya kuwabaini wale wote waliowageuza wanafunzi wa kike kama wake zao.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha waalimu Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambapo amesema kuwa amewaagiza Wakurugenzi wake kuhakikisha wanapita kila shule na kupigisha kura kwa wanafunzi kuwabaini walimu wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi wa kike na kiume.

Aidha amefikia hatua mara baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya waalimu wa kiume na wakike wanaojihusisha kimahusiano na wanafunzi katika shule mbalimbali wilayani humo.

Hata hivyo, amewataka wakurugenzi wote kusimamia zoezi hilo kikamilifu ili kuweza kuondoa tatizo hilo ambalo limekuwe likichukuwa nafasi kubwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele.

Video: Serikali yajibu mapigo, Acacia wafunguka kesi kuidai Serikali
TUCTA: Waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki walipwe