Wakazi wa Mitaa ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,mjini Kibaha wameanza kujitolea kujenga kivuko cha muda kuvuka mto Mpiji ili kuepukana na maafa ya kujeruhiwa na mamba kutokana na kero kubwa ya ukosefu wa kivuko cha kudumu .
 
Kufuatia jitihada hizo ,mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvester Koka amechangia milioni tatu ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.
 
Akikagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho cha kuvuka mto kwenda Kibwegere Kibamba jijini Dar es salaam ,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni humo, Koka amesema kuwa wakati wakielekea kwenye mkakati mkubwa, hakuna budi kuanza na mkakati wa muda mfupi .
 
Aidha, amesema kuwa serikali kupitia wakala wa barabara mijini ( TARURA ) imetenga shil. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko hicho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kujenga kivuko kikubwa na cha kudumu.
 
“Nilipiga kelele kuhusu kivuko hiki na kimeitikiwa na TARURA, kuna mpango wa kujengwa ambapo imeshatengwa mil 500 ila tatizo lililopo ni mvutano kati ya TARURA Kibamba na Kibaha jambo ambalo linafanyiwa kazi,”amesema Koka
 
  • Nikisema Sukuma ndani sitanii, sasa naanza nawewe- RC Tabora
  • NEC yatoboa siri ya wabunge waliohama Chadema kupita bila kupingwa
  • Iwe kwa kutumwa au makusudi Ushoga ni mwiko Tanzania- Kangi Lugola
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa nia yake ni kuona kivuko cha kudumu lakini wakati mambo hayo yakiendelea kufanyiwa kazi, amewaomba wahusishe wataalamu katika harakati hizo ili kuondokana na hasara ya kujenga kisha kivuko kusombwa na maji ya mvua mara kwa mara.

Moto waua makumi, 250,000 wakimbia makazi
Habari Picha: Kikao cha maandalizi ya manunuzi ya Korosho