Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wale wote watakaosababisha kuibuka kwa hoja za ukaguzi wa hesabu za serikali katika Halmashauri zao.

Zelote amesema hayo alipohudhuria kwenye baraza maalum la madiwani la kujadili na kujibu hoja 147 za mkaguzi wa hesabu za serikali nchini kwa mwaka wa fedha 2015/2016 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Amesema kuwa kila mamlaka ya nidhamu ichukue hatua za kinidhanmu kwa mujibu wa sharia kwa watumishi ambao wamesababisha hoja za ukaguzi kwa uzembe au kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na taarifa juu ya hatua hizo apelekewe.

“Kwenye hoja zilizojibiwa ningependa sana hoja ziwe na data zinazoeleweka na za uhakika, na kuacha kitu kinachoitwa tunaendelea kuishughuilikia, iseme tumefikia wapi, sio tunaendelea, Hakuna kinachoendelea, lazima kupiga hatua kuondoka kwenye hoja hiyo, nimesikia kuwa kuna watu wamechukuliwa hatua lakini sijaziona,” Mh. Zelote alibainisha.

 

McGregor amvaa Tyson, adai atakula maneno yake
Kambi ya Maalim Seif yatangaza mkakati wa kujibu ‘timuatimua’ ya Lipumba