Mtandao maarufu wa WhatsApp umepiga marufuku watu walio chini ya umri wa miaka 16 kutumia mtandao huo, kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.

Kabla ya hapo watumiaji walitakiwa kuwa na umri wa miaka 13, lakini sasa watumiaji ni lazima wawe na miaka 16 na kuendelea kulingana na utaratibu mpya wa  kulinda taarifa binafsi Barani humo.

Aidha, mtandao huo ambao unamilikiwa na mtandao mkubwa wa facebook, utawauliza watumiaji kuthibitisha umri wao watakapo jisajili kuanzia mwezi ujao mwaka huu.

Hata hivyo, kutokana na hilo WhatsApp utakuwa mtandao wa kijamii wa tano kuhitaji umri maalum ili kuweza kuutumia, ikiwemo Facebook, Snapchat, Instagram na YouTube.

 

Watu 9 wakamatwa wakiandamana Posta, Dar es Salaam
Zlatan Ibrahimovic hatokwenda Urusi