Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imesikiliza kesi ya mauaji namba moja ya mwaka 2019 dhidi ya Jamhuri na watuhumiwa watatu waliohusika na mauaji ya watoto watatu katika kijiji cha Ikando Kata ya Kichiwa wilayani Njombe.

Akisoma kesi hiyo mbele ya mahakama Wakili mwandamizi wa serikali, Ahmed Seif amesema kuwa mtuhumiwa namba moja, Joel joseph Nziku mbena (35)dereva anaishi Magegere mjini Makambako, mshatakiwa namba mbili Nasson Alfredo kaduma (39) mkulima anaishi kijiji cha Ibumila na mtuhumiwa namba tatu Alphonce Edward Danda (51)naye anaishi katika kijiji cha Ibumila wote wanashtakiwa kwa makosa matatu ya mauaji.

Aidha, amesema kuwa kosa la kwanza ni mauaji kifungu cha sheria 196 na 197 vya kanuni ya adhaabu sura ya 16 marejeo ya 2002, mnamo tarehe 20 mwezi wa kwanza mwaka 2019 kijiji cha Ikando kata ya kichiwa tarafa ya Makambako wilayani Njombe kwa pamoja walihusika kumuua Godliver Nziku kosa la pili washtakiwa walihusika kumuua Gasper Nziku na kosa la tatu washatakiwa wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kumuua Giriad Nziku.

Kwa upande wake hakimu mkazi mkoa wa Njombe, Magdalena Mtandu amesema kuwa hayo ndio makosa yao na hawapaswi kujibu lolote huku wakirudishwa rumande na kusubiri tena hadi tarehe 25 ya mwezi wa pili mwaka 2019 kesi hiyo itakapo tajwa tena.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 13, 2019
CCM Njombe waeleza siri ya mafanikio mbele ya viongozi wa Kitaifa

Comments

comments