Usiku wa Nov 28, 2021, umeingia kwenye kitabu cha historia nyingine za matukio makubwa aliyowahi kuyafanya msanii Wizkid huko London Uingereza.

Wizkid ametumbuiza mbele ya mashabiki takribani elfu ishirini walioujaza uwanja maarufu nchini humo ‘The O2 Arena’.

Licha ya makubwa ambayo ni kawaida kupatikana kwenye shows zake, kivutio kingine kilicho konga nyoyo za wengi kwenye show hiyo, ni pale ambapo Wizkid alimpandisha msanii Chris Brown jukwaani kama suprise kwa mashabiki waliohudhuria.

Wakati akimpandisha jukwaani alizungumza maneno kadhaa ya utambulisho akimtaja Chris Brown kama mtu wa kwanza kumuonyesha upendo na kumuunga mkono alipoanza kuingia rasmi kwenye soko la muziki Kimataifa.

“Huyu ni ndugu yangu kwa zaidi ya miaka kumi, huyu ni mtu wangu, mtu wa kwanza kunionyesha upendo muda wote, nilipoanza kuingia Kimataifa”. Alisema Wizkid.

Kwa kipindi cha miaka kumi ya ukaribu wa msanii Wizkid na nyota huyo wa Marekani Chris brown, wamefanikiwa kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye wimbo wa pamoja uitwao ‘African Bad Gyal’ ambao uliachiwa rasmi mnamo mwaka 2017.

TARURA yatoa elimu kwa wakusanya ushuru Dar es Salaam
Uamuzi kesi ya Mbowe na wenzake leo