Klabu ya Brighton and Hove Albion imemsajili kiungo kutoka nchini Mali Yves Bissouma akitokea Ufaransa kunako klabu ya Lille, kwa mkataba wa miaka mitano.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, ameshaitumikia timu ya taifa ya Mali katika michezo 13, na kwa upande wa Lille amecheza michezo 55 baada ya kupandishwa katika kikosi cha kwanza mwaka 2016.

“Ni mtu mwenye uwezo mzuri kiufundi anapokua uwanjani, ana uwezo wa kumiliki mpira na kuchezesha timu,” amesema meneja wa Brighton Chris Hughton alipohojiwa na mwandishi wa tovuti ya klabu hiyo.

Bissouma amesajiliwa kwa ada ya Pauni milioni 17, ambayo inaweka rekodi klabuni hapo.

Bissouma anakua mchezaji wa sita kusajiliwa katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi, na anaaminiwa ataweza kuleta changamoto mpya ambayo itaiwezesha Brighton kuimarika na kumaliza ligi katika nafasi za juu, tofauti na ilivyokua msimu uliopita, ambapo walimaliza kwenye nafasi ya 15.

Liverpool Kumng'oa Alison Stadio Olimpico?
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 18, 2018

Comments

comments