Takriban watu 19 wamefariki, na wengine 12 wakiwa wamelazwa Hospitalini baada ya kunywa pombe yenye sumu kwenye Duka moja lililopo pembeni ya barabara kaskazini mwa nchi ya Morocco.
Kurugenzi ya Usalama wa Taifa (DGSN), imesema katika taarifa yake kwamba Polisi imemkamata mshukiwa (48), kuhusiana na tukio hilo huku waathiriwa wakihisiwa kunywa pombe hiyo yenye sumu katika duka la mshukiwa, ambapo lita 50 za kioevu hicho zilikamatwa.
Afisa wa Wizara ya Afya aliwaambia waandishi wa habari kuwa miili ya waathiriwa tisa ilipokelewa Hospitalini na idadi ya waliofariki iliongezeka hadi 19 hapo jana Septemba 28, 2022.
Muuguzi wa Hospitali ya Ksar El Kebir, alisema watu 30 walipelekwa hospitalini hapo wakiwa katika hali mbaya, na wawili wakiwa katika uangalizi maalum na manusura walisema wanahisi kupata maumivu ya kichwa, kutapika na tumbo kuuma, huku aliambia vyombo vya habari.
Sheria ya Morocco, inakataza uuzaji wa pombe kwa Waislamu, lakini inapatikana kwa urahisi katika baa, migahawa na maduka ambayo hutoa kwa busara kwa ajili ya kuuzwa nyuma ya madirisha opaque au mapazia mazito, ambapo Julai 2021, takriban watu 20 walikufa katika tukio kama hilo huko Oujda, mashariki mwa Moroko.