Ikiwa unataka kupunguza uzito unaweza jaribi kupunguza kalori ingawa lakini kula kidogo pia kunaweza weka afya yako hatarini. Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa mlo wa chini ya kalori 1,000 kwa siku kwa ujumla hushindwa kutoa lishe bora ambayo mwili wako unahitaji, na inaweza kusababisha upungufu wa vitamini na madini unaohusishwa na masuala ya kiafya.

Ulaji wa kalori chache kuliko ivyohitajika husababisha mwili wako kudhohofisha misuli na uchomaji wa mafuta mwilini, ambapo kadri unavyokuwa na tishu kidogo, ndivyo kasi yako ya kimetaboliki inavyopungua, ambayo haitafaa kwani utapoteza uzito, ambapo leo tumekuandalia njia rahisi za kupunguza uzito.

Lakini hebu tuangalie kwanza unene husababishwa na nini hasa. Unene husababishwa na mambo mengi ikiwemo ulaji uliopitiliza zaidi ya mwili unavyohitaji, kwani mwili baada ya kuchukua hitaji lake huifadhi mabaki kama mafuta, na kadri unavyokula zaidi vyakula vya mafuta ndivyo unavyoongeza mafuta.

Unene pia husababishwa na kutofanya mazoezi ya kutosha, mfumo wa umeng’enyaji chakula kutofanya kazi vizuri, kula vyakula vinavyozorotesha uharakishwaji wa mfumo wa umeng’enywaji kama maziwa au nyakati za usiku au unywaji wa maji ya baridi baada ya chakula, lakini mbinu hizi zinaweza kuwa msaada kwako.

1. Asali na Mdalasini

Chemsha Asali na Unga wa Mdalasini kwa kipimo cha kikombe kimoja cha maji na unywe kila siku asubuhi, kabla ya kula chochote na usiku kabla ya kulala. Hiyo huweza kupunguza uzito hata ukiwa mnene sana na pia inashauriwa unywe mara kwa mara, ili kuzuia mafuta mwilini.

Sharubati ya Limao na Asali

Asali na limao zote zinakemikali itayokusaidi kurahisisha umeng’enywaji kufanyika haraka hivyo utaweza kusikia njaa baada ya muda Fulani (huwenda ikawa ni mapema kuliko kawaida). Ikiwa utaendelea kula kila usikiapo njaa tiba hii haiwezai kukusaidia lolote.

Ni lazima wakati Fulani tumbo lako liwe tupu, ili mwili utumie ziada ya chakula ulichohifadhi kama mafuta. ambapo juice ya limao na asali zote zinasaidia kuifanya fati iliyopo mwilini mwako kutumika, kama utahisi njaa jizuie kula kila mara pia jizuie kula vyakula nyenye mafuta mengi kama vibanzi vilivyochanganywa na mayai, nyama choma ya mbuzi, supu nk.

Faida nyingine ya juce ya limao na asali inasaidia kuuwa bakteria ambao wanazorotesha mfumo wa chakula na utoaji taka kufanya kazi vizuri na ili kusaidia ufanyaji wa kazi vizuri basi kunywa maji ya kutosha ikiwezekana ya vuguvugu.

JKT Tanzania kuingia sokoni Dirisha Dogo
Mourinho: Ninatamani Arsenal itwae ubingwa