Wizara ya Kilimo ya Malawi imepiga marufuku uagizaji bidhaa kutoka nje ikilenga Nchi za Tanzania na Kenya, kufuatia taarifa yake inayosema hatua hiyo inatokana na ugonjwa wa Mahindi unaosababishwa na Lethal Necrosis ambao hauna tiba.
Malawi imesema ina wasiwasi wa kuenea kwa ugonjwa huo wa Mahindi, ambao unaweza kuharibu chakula kikuu kinachotegemewa nchini humo ambapo zaidi ya watu wake milioni 4 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Kenya na Tanzania kwa muda mrefu zimekuwa vyanzo vikuu vya mahindi kwa Malawi wakati wa uhaba wa chakula, huku mtaalamu wa kilimo katika Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Sera ya Chakula, Henry Kamkwamba amesema marufuku hiyo ni tahadhari kwao.
Hata hivyo, Wizara ya Kilimo ya Malawi ilitangaza marufuku wiki hii ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje katika taarifa inayosema ugonjwa wa Mahindi unaosababishwa na Lethal Necrosis hauna tiba na unaweza kusababisha hasara ya mavuno kwa asilimia 100.