Hakuna shaka kwamba endapo utafika jiji la Bandar Seri Begawan (Dar us salam), nchini Brunei utakubaliana nami kuwa hiyo ni mojawapo ya nchi tajiri zaidi Duniani, ikiwa na pato la juu zaidi kiuchumi na mahali pa kupendeza ambapo kila binadamu angependelea kuishi.

Katika Taifa hilo linaloongozwa kifalme, Dhahabu hupatikana kirahisi kwani kuna miamba mikubwa ya Dini hilo adimu ambalo kwa baadhi ya maeneo huonekama hata kwa macho na usiweze kuamini uhalisia wa unachokiona.

Katika Taifa hilo, mshahara wa chini kabisa ni dola 25 kwa siku ambayo ni sawa au zaidi ya Shilingi 50,000 kwa siku kulingana na bei ya dola, huku ukosefu wa ajira ukiwa ni wastani wa asilimia moja na Serikali hulipa gharama zote muhimu na mfanyakazi halipi kodi yeyote na Nchi haina deni.

Elimu katika Taifa hilo ni bure na watoto chini ya miaka 12 hutibiwa bila malipo huku watu wazima wakilipia dola moja pekee kwa matibabu na kiwa hakuna tiba ya ugonjwa unaougua Serikali itakugharamia safari na matibabu nje ya nchi, yaani kama ukifika utagoma kurudi.

Paza sauti: Simu zisiwaendeshe Madereva
Maxime afunguka killichomng’oa Kagera Sugar