Dunia ina mambo mengi sana ambayo mengine si rahisi kuyafahamu lakini yapo ya kushangaza na yenye historia, ikiwemo Bahari iliyokufa ikifahamika kama ‘Dead Sea’ iliyopo Mashariki ya kati.

Katika Bahari hiyo mtu ukiingia huwezi kuzama hata kama hujui kuogelea na si rahisi kuamini kwamba kuna Bahari au Ziwa lolote duniani ambalo mtu akiingia hawezi kuzama lakini kwa Dead Sea ni tofauti, kwani hilo linawezekana.

Si ajabu sana kukuta au kuona watu wakiingia katika maji ya Bahari hiyo mfu wakielea huku wakisoma magazeti, katika Bahari hiyo iliyoitwa hivyo kutokana na ukweli kwamba maji yake yana chumvi nyingi mno kiasi kwamba viumbe vyenye uhai haviwezi kuishi ndani yake.

Kama ujuavyo tuna lugha nyingi Duniani, hivyo wakati sisi tukiita Bahari mfu kule Uarabuni  wanaiita “al-Bahr al-Mayyit” na kwa Kiyahudi inaitwa “Yam Ha-Mela” yote yakimaanisha “Bahari ya Chumvi” na licha ya eneo hilo la Maji kuitwa Bahari, lakini ukubwa wake ni kama Ziwa la kawaida.

Bahari hiyo, ambayo pia huitwa Salt Lake yaani “Ziwa la Chumvi”, iko katikati ya Jordan kwa upande wa Mashariki ikipakana na Israel upande wa Magharibi na Palestina kwa Upande wa Magharibi.

Uso wake na kingo zake ziko mita 422 chini ya usawa wa bahari, ambacho ni kipimo cha chini zaidi katika uso wa dunia katika eneo lililoko katikati ya ardhi kavu maji yake yakiwa na chumvi kwa asilimia 33.7, japokuwa Ziwa Assal lililoko Nchini Djibouti na maziwa ya McMurdo Dry Valleys ya eneo la Antarctica yenyewe yana viwango vya juu zaidi vya chumvi.

Lakini ‘Dead Sea’ ina kiwango cha chumvi ambacho ni mara 8.6 zaidi ya kile kilichomo katika bahari, hivyo wingi huo wa chumvi ni moja kwa moja hauwezi tena kuruhusu viumbe hai kuishi ndani yake na ndiyo maana ikaitwa Bahari iliyokufa.

Hata hivyo, kuna aina fulani za bakteria na mimea ambayo huweza kuishi katika maji hayo kwani mazingira ya Dead Sea yako sawa kabisa na ziwa liitwalo Great Salt Lake lililopo Utah, Nchini Marekani.

Urefu wa ziwa hilo ni kilomita 67 na upana wake (katika sehemu ndefu zaidi) ni kilomita 18, na mto pekee unaomwaga maji ndani yake ni Mto Jordan huku uzito wa maji yyakeukiwa ni kilo 1.24, jambo ambalo linafanya uogeleaji ndani yake kuwa mgumu, lakini maji hayohayo hutoa burudani tosha.

Unaweza jilaza juu yake ukabaki unaelea muda wote huku ukifanya msmbo yako mengine kama kusoma gazeti au kunywa kinywaji bila kuzama na maajabu ya bahari au ziwa hilo, ambalo katika Biblia, linatajwa liliwahi kuwa makimbilio ya Mfalme Daud ni kwamba imekuwa ikivutia maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Dead Sea ni moja ya vituo vya mwanzo duniani vya tiba tangu enzi za mfalme Herode na miongoni mwa bidhaa zinazopatikana katika bahari hiyo ni chumvi za aina ya “potash”, mbolea, Dawa za kuhifadhi viumbe aubvitu ili visioze.

Hapo pia kuna nadharia kwamba kiasi cha miaka milioni tatu iliyopita, leo imekuwa ni bonde la Mto Jordan, Dead Sea na Wadi Arabah lilikuwa kila mara linafurika maji kutoka Bahari ya Mediterranean na yakifika hapo yalitokea kupitia Bonde la Jezreel.

Mafuriko hayo, yalikuwa yakilikumba eneo hilo na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa na matokeo yake ni kwamba ziwa ambalo lilikuwa katika eneo la Dead Sea, ambalo liliitwa “Ziwa Sodoma”, lilibakia na marundo ya chumvi ambayo unene wake ukafikia kilomita tatu.

Baada ya mafuriko hayo kukoma, eneo hilo likabaki na maji na chumvi na kufanya leo hii kuwa Dead Sea enwo ambalo pia ni kituo kikubwa cha tiba kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ya ngozi.

Ally Kamwe: Tunatumia akili kubwa, mtatuelewa
Wawili kuongeza nguvu Dodoma Jiji FC