Wizara ya Kilimo kupitia Wakala wa mbegu – ASA, inatarajia kusambaza Tani 2,045 za mbegu bora zilizothibitishwa ubora, ikijumuisha tani 700 za mbegu chotara ambazo zinaingizwa kutoka nje ya nchi na tani 625.4 za makampuni binafsi Nchini.

Aidha, Usambazaji wa mbegu bora kwa mfumo wa ruzuku umeongeza uzalishaji  wa alizeti nchini ambapo kwa msimu huu wa 2023/24 uzalishaji wa alizeti umefikia tani 1,100,000 ikiwa ni ongezeko kutoka Tani 400,000 zilizovunwa mwaka jana 2022/23.

Tayari Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amezindua usambazaji wa mbegu za ruzuku za Alizeti kwa Wakulima katika msimu wa 2023/24 uliofanyika Mkoani Singida.

Akizindia mpango huo, Silinde amesema, “Serikali inatambua gharama za uzalishaji na usambazaji mbegu na changamoto ya mbegu kuwafikia Wakulima kwa wakati, hivyo kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo, Wizara inaendelea kuondoa changamoto hizo kwa kuwafikishia mbegu kwa wakati kupitia Halmashauri mbalimbali.”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 5, 2024
Mapato chanzo anguko la Uongozi Mnada wa Pugu