Dunia haituachi salama, na vituko Duniani haviwezi kuisha kiukweli, yaani kila mtu anaamini lake na ni ngumu sana kuwabadili binadamu na ukikaa vibaya unaweza badilishwa wewe.
Sina shaka unamfahamu Mamba na balaa lake, mara kadhaa zimeripotiwa kesi kwamba wanauwa watu na hata wengine kusababishiwa ukilema. Mamba pia anatajwa kama kiumbe hatari wa majini.
Sasa kuna eneo linaitwa Bazoule linapatikana nchini Burkina Faso, hapo Mamba si viumbe hatari kabisa na kwa jamii ya eneo hilo, yaani huwachukulia Mamba eti kama viumbe watakatifu.
Katika eneo hilo, ikitokea Mamba ameaga dunia basi huzikwa kwa heshima zote kamą ile anayopewa Mwanadamu na msiba hutengwa kabisa, ili kuomboleza.
Na utaratibu wao wa maisha watu wa Bazoule, umewafanya kuwa na tamasha liitwalo ‘Koom Lakre’ linalofanyika mara moja kila mwaka likisheheni Mambo mbalimbali na Mamba huwa ndiyo Habari kuu.
Wakati wa tamasha hili, watu hukusanyika kwa wingi ili kudumisha mila na pia kupata baraka toka viumbe wangine wanaowaamini ikiwemo mpendwa wao Mamba.
Makala: Hivi ni kweli Kuku alipanda Baiskeli
Hata hivyo, Mamba hao wa Burkina Faso inasemekana pia wanapatikana eneo la Paga la Nchini Ghana.
Inaarifikwa kuwa jamii ya watu wa Paga nao wanawaona Mamba ni viumbe watakatifu wakiaamini kwamba wana roho kama za Binadamu, hivyo nao eti wanawaabudu na hata kuwapa salaam.
Wakati nilikuwa mdogo, niliwahi kuwasikia Wazee wakisema kuwa uyaone, me nilidhani ni maghorofa nikaitia kwa bashasha ‘sawa’ huku nikiulaumu utoto…… ni bora ningebaki kulekule utotoni.