Korosho ghafi kiasi cha Tani 150,000 zimesafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kutumia Bandari hiyo kusafirisha korosho zote ghafi zinazolimwa Katika Mikoa ya Kusini ikiwemo Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema tangu kuanza kwa msimu wa Korosho Bandari hiyo imehudumia Meli zaidi ya 18 za makasha, tatu zilizoleta makasha matupu na 15 zilizosafirisha Korosho ghafi.

Amesema, “tumeshasafirisha tani 150,000 na mpaka mwishoni mwa Januari tutakuwa tumeshasafirisha tani 200,000. Tunakushukuru sana Serikali kwa maelekezo yake ambayo yameongeza ufanisi wa Bandari.”

Hata hivyo, Nyathi pia amewashukuru Wadau wa Bandari na kampuni ambazo ziliamua kuwekeza katika Bandari hiyo ikiwamo Kampuni ya kuhudumia Makasha ya CMA na Kampuni ya Meli ya Mediteranian Shipping na kusafirisha Korosho hizo ghafi.

Try Again: Tunaendelea kushusha watu kazi
Young Africans yatuma salamu Algeria