Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amekutana na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Alfred M. Sears pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM), unaoendelea jijini Kampala, Uganda.

Katika kikao hicho, Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele, ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, Biashara na Uwekezaji, michezo na utamaduni.

Mapema hapo jana Januari 17, 2024, Waziri Makamba pia alikutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Jamhuri ya Kenya, Dkt. Musalia Mudavadi jijini Kampala na kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Mataifa yao na kuahidi kuendelea kutumia majukwaa ya kidiplomasia kutatua changamoto mbalimbali.

Changamoto hizo ni pamoja na zile zinazokwamisha ustawi mzuri wa Biashara, uwekezaji, utalii na uendelezaji wa miundombinu kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kiungo KMC FC amfagilia Zouzoua
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 18, 2024