Inawezekana kabisa ukawa ni wale Binadamu ambao huwa hawana urafiki na Paka, lakini nina uhakika huwezi kumshinda Papa Gregory IX aliyeongoza Kanisa hilo kuanzia Machi 19, 1227 hadi kifo chake mwaka 1241, ambaye inadaiwa alikuwa na makasiriko makubwa dhidi ya mnyama huyu rafiki wa Wanadamu.
Katika kipindi hiki, Watu walikuwa na imani haba kuhusu ulimwengu, ambapo Papa huyu Gregory aliamini kwamba paka walibeba roho ya Shetani na kwa hatua hiyo hawakupaswa kabisa kuaminiwa akisema wana ushirikina na hasa Paka Weusi wao humkosesha mtu bahati na kuwaaminisha wafuasi wake.
Inaarifiwa kuwa, kati ya mwaka 1233 na 1234, Gregory ambaye alikuwa ni Kiongozi wa Kanisa Katoliki, alikuwa na mamlaka makubwa kwa utawala wake, na katika imani yake aliamini pia katika jambo jingine kuwa kwamba Paka walikuwa ni mawakala wa Shetani na hivyo kudai kuwa Shetani ni muharibifu wa maisha ya Wanadamu na hivyo uharibifu wowote ni dhambi na chukizo mbele za Mungu.
Hapo, Papa Gregory IX akaita kikao na kuamuru kwamba Paka wote wanapaswa kuangamizwa. Hiyo ilikuwa ni amri kama unavyofahamu Mkuu anapotoa agizo ni lazima litekelezwe na hivyo likapokelewa na mikakati ya vita dhidi ya Paka ikaanza na mauaji makubwa ya Paka yakafuata na kupelekea kuzuka ugonjwa tauni uliowashambulia watu wengi kwani hapakuwa na Paka ambao wangeweza kuua Panya.
Panya hao walikuwa na Viroboto ambavyoo vilisababisha ugonjwa huo na hivyo walipotokea Wagonjwa wengi wa Tauni watu waliamini kuwa ni kweli Panya wana ushetani kwani wamewasababishia madhara kiafya ingawa vita hivyo vya Papa dhidi ya Paka havikuwaathiri Paka pekee, kwani watu waliteseka pia.
Maelfu ya watu hasa wanawake, walikuwa wakishutumiwa na kunyanyaswa na majirani na marafiki na kazi mpya ilikuwa imezinduliwa ya kuwinda Mchawi kwani Watu wa kidini waliotaka kuthibitisha uaminifu wao kwa Kanisa waliwawinda na kuwashutumu wanawake kwa uchawi, huku wanawake wasio na hatia wakiteswa na kuuawa.
Kwa hatua hii, Paka bado hawakuwa salama, ingawa wakati huu Paka walikuwa wakiuawa kwa sababu ya pili ambayo ni uwindaji wa Wachawi na ilipofika mwishoni mwa miaka ya 1400, Paka sasa wakawa wakiuawa kwa sababu waliaminika kuwa jamaa wa wachawi na badaye Papa akaona vita ni kubwa na ina madhara.
Akakaa chini na kutafakari upya na hapo akaona apotezee na mauaji ya Paka rasmi yalikoma. ingawa ushirikina bado unaendelea hadi leo, lakini hii inaonesha kwamba baadhi ya mawazo ya hofu au kuhisi yanaweza kupelekea ukweli na yakaleta madhara kama ambavyo yalitokea wakati wa utawala wa Papa Gregory IX .
Itakumbukwa kuwa, hata huko Elizabethan Nchini Uingereza, wakati wa kutawazwa kwa malkia picha ya Paka ilichomwa moto hali iliyowafanya Wanyama hao kuwa na wakati mgumu katika baadhi ya vipindi vya historia, ingawa sasa wamesalimika na wanaendelea ‘kula utawala’ wakiji ‘selfie’ kama inavyoonekana pichani.