Watalii kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kushanganzwa na aina ya vivutio vilivyopo majini katika Hifadhi ya Taifa Saadan kwenye fukwe za bahari ya Hindi, ambapo hifadhi hiyo imegawanyika katika maeneo mawili Nchi kavu asilimia 30 na majini asilimia 70 jambo ambalo linachangia kuvutia Watalii kutokana na aina mbalimbali za Viumbe hai vilivyopo
Uwepo wa aina tofauti za Viumbe maji ikiwemo kamba mti na miamba ya kipekee ya mazalia ya samaki katika kisiwa cha Mafui San Bank kinachopatikana katikati ya bahari ya Hindi kumeendelea kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali na kuifanya hifadhi hiyo kuendelea kuwa maarufu duniani.
Hayo yameelezwa na Mwongoza watalii Hifadhi ya Saadan, Hamis Mwinyikombo ambaye amesema silimia 70 katika hifadhii ya sadani ni eneo la nchi kavu na asilimia 30 ikiwa ni eneo la bahari, ya hindi na kusiaiatiza kuwa uwepo wa Vivutio tofauti tofauti vya kitalii katika hifadhi ya saadan kunandelea kuwavuti watalii wengi zaidi kukiwa kunachagizwa na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika sekta hii ya utalii.
Amesema watalii wengi upendelea kutembelea kisiwa cha Mafui San Bank na hii inatokana na uwepo wa miamba tofauti tofauti ya matumbawe yanayotumiwa na viumbe mbalimbali kuzaliana pamoja na uwepo wa fukwe inayotumiwa na kasa wa kijani kuzaliana.
Mwinyikombo ameongeza kuwa, katika hifadhi ya saadani Miongoni wa Vivutio vya kipekee ni uwepo wa kisiwa cha Mafui San Benk ambacho watalii wengi ufika na kwenda kukiangalia mbapo maji yake upya na kujaa nakuacha mchanga unaovutia katika kisiwa hicho.
Kutokana na umuhimu wa hifadhi hiyo ya Saadan Afisa Uhifadhi Mwandamizi katila Hifadhi ya Taifa ya saadan Prisca Eliasia amesema mikakati mbalimbali ya kuendelea kupokea wageni wengi zaidi inaendelea kuwekwa katika kipindi hiki cha Mwezi wa wapendanao ambapo amesisitiza watanzania Kutembelea Hifadhi hiyo na ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo.