Lydia Mollel – Morogoro.

Moja ya njia sahihi ya utunzaji wa mazingira ni kupanda kwa wingi kama alivyofanya Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Alex Mkama kwa kuongoza Maofisa Wakaguzi na Askari katika zoezi la Upandaji miti katika kambi za Polisi pamoja na makazi jirani Februari 10, 2024.

Katika zoezi hilo, Mkama amesema Mkoa wa Morogoro jumla ya miti 500 imepandwa na zoezi hilo linafanyika Tanzania nzima kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi IJP Camilius Wambura pamoja na Serikali hivyo hawanabudi kuyatekeleza  kwa ukubwa wake.

Amesema, zoezi la kupanda miti kwa Askari wa Mkoa wa Morogoro litaendela wiki nzima katika maeneo mbalimbali ikiwa nikuadhimisha siku ya Mwanamke duniani ambayo kilele chake ni Machi 8, 2024.

Zoezi hilo, limeshirikisha Wachezaji wa mpira wa miguu ya Mbeya city inayoshiriki ligi ya Championship ambao wanaofanya mazoezi kwenye uwanja wa Polisi uliopo kwenye kambi za Polisi Morogoro.

Mmoja wa wachezaji hao, Pius Joseph amesema ni mara ya kwanza wanaalikwa na Jeshi la Polisi kushiriki zoezi la kijamii kwao imekuwa faraja na imewapa nguvu ya kwenda kupambana na kupata ushindi kwenye mchezo wao unaofuatia.

Wananchi toeni maoni kwa ajili ya sera yenye tija - Waziri
Viumbe hai Majini Hifadhi ya Saadan vyawashangaza Watalii