Abel Paul, Jeshi la Polisi – Arusha.

Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini (STPU), kikiongozwa na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi, Simon Pasua kimeshiriki katika kampeni ya upandaji miti zaidi ya elfu moja katika Kata ya Monduli Juu Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha, ambayo ilizinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP. Camillus Wambura.

Akiongea mara baada ya zoezi la upandaji Miti, Kamanda Pasua amesema kwa kushirikiana na wananchi watahakiksha Mazingira yanabaki salama na kwamba wataweka jitihada katika kutunza mazingira.

Amesema, Wananchi hao wanatakiwa kuendelea kutoa taarifa za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo, huku akitoa wito kwa Wafugaji kufuata sheria na taratibu za usafirishaji wa mifugo nje ya nchi na kusisitiza kuwa wale watao kiuka watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Monduli Juu, Thomas Meiyan amesema Wananchi wa Monduli wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi huku akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu hassan kwa namna alivyo toa fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya kata ya Monduli juu.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Emairete, Upendo Machanja amesema miti hiyo itakuwa chachu ya ufaulu na maendeleo ya kitaaluma kwa ujumla, kwani shule hiyo ilikuwa na uwazi ambao unakwenda kuisha baada ya miti hiyo kustawi.

Mmoja wa Wanafunzi wa shule hiyo, Zawadi Kituya amesema miti hiyo itabadilisha mwonekano wa shule yao na wataitunza vizuri ili iwasaidie kitaaluma, huku Mwenyekiti wa Kijiji cha Emairete Kata ya Monduli Juu, Mboyo Kaileza akisema tayari wameshauriana kutoingiza mifugo yao katika eneo hilo lililopandwa miti zaidi ya 1,000.

Viongozi wapewa neno Kampeni Chanjo ya Surua, Rubella Mbeya
Serikali yaanza utekelezaji mradi wa Maji Dambia - Haydom