Serikali Nchini, imezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza jukumu lao la kuhakikisha taka zote katika maeneo yao zinakusanywa na kutupwa katika madampo yaliyopo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo wakati akichangia taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, kila halmashauri nchini ni lazima iweke utaratibu mzuri wa zoezi la uzoaji wa taka ngumu na si kuziacha zikizagaa ovyo kwenye mitaa hali
inatoweza kusababisha magonjwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo.

“Nashukuru kuna yale madampo matano yaliyojengwa katika mikoa mbalimbali kupitia mradi lakini baadhi ya halmashauri bado zinasuasua katika
ukusanyaji wa taka..utakuta mtu amepewa tenda (zabuni) halafu hilo lori lenyewe analotumia ni takataka, hili haliwezekani lazima tufikie mahali
tutumizi majukumu yetu,“ amesema.

Dkt. Jafo ameongeza kuwa, Ofisi ya Makamu wa Rais jukumu lake ni kusimamia sera wakati halmashauri hizo zinapaswa kutekeleza jukumu lao la
kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi.

 

Watoto 700,000 hatarini kupata utapiamlo - UNICEF
Ukiukwaji kanuni za maadili: Madaktari tisa hatiani