Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa – UNICEF, limesema jumla ya Watoto 700,000 nchini Sudan wapo hatarini kukumbwa na utapiamlo mbaya zaidi kwa mwaka huu wa 2024, ambapo huenda wengi wao wakapoteza maisha.

Msemaji wa UNICEF, James Elder, amesema endapo msaada wa ziada wa shirika hilo hautatolewa, ni wazi kuwa hawataweza kuwatibu zaidi ya watoto 300,000 kati ya wale wasiofikiwa vyema, na kwa hivyo makumi ya maelfu huenda wakafa.

Amesema, zipo pia aina mbaya zaidi za utapiamlo ambao unamfanya mtoto awe na uwezekano mara kumi wa kufa, kutokana na maradhi kama vile Kipindupindu na Malaria.

Februari 8, 2024 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres aliayahimiza mataifa kutowasahau raia waliozingirwa katika vita vya Sudan na kutoa maombi ya dola bilioni 4.1, ili kushughulikia mahitaji ya Kibinadamu.

 

Kamati ushiriki wa Wazawa Miradi ya Ujenzi yapewa mwezi
Maagizo ya Dkt. Jafo kwa Mamlaka Serikali za Mitaa