Chanzo cha ajali ya msafara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda kupata ajali ya magari zaidi ya saba tisa kugongana kilometa chache kabla ya kufika Wilayani Masasi ukitokea Ruvuma kimetajwa kuwa ni breki za ghafla zilizofungwa na gari aina ya Toyota Prado ikidaiwa kuwa Dereva wake aliona roli mbele ya msafara.

Ajali hiyo ilitokea alasiri ya Februari 11, 2024 wakati msafara huo ukielekea Mkoani Dar es Salaam baada ya Makonda kutangaza kusitisha ziara yake mkoani Ruvuma, kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.

Katika ajali hiyo, inaarifiwa kuwa watu saba walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Masasi na ilitokea katika barabara iliyokuwa kwenye matengenezo hivyo kufanya vumbi kuwa jingi na kutowezesha kile kinachoonekana mbele.

Ongezeni kasi kukuza uchumi wa Taifa - Nderiananga
Dkt. Molle aionya jamii matumizi holela ya P2