Kiongozi wa chama cha ACT – Wazalendo Taifa ndugu Zito Kabwe, amesema kwamba masuala ya migogoro ya ardhi, mipaka kati ya wafugaji na hifadhi za taifa na vijiji , kupanda kwa gharama za maisha pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana ni miongoni mwa changamoto kubwa Tanzania inayoweza kuleta madhara makubwa iwapo hatua thabiti za kukabili hali hiyo hazikuchukuliwa.
Zito ameyasema hayo katika ofisi Kuu za Chama hicho zilizopo Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam alipofungua mkutano wa Halmashauri Kuu taifa ya chama hicho kwa ajili maandalizi ya Mkutano mkuu wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezizi ujao.
Amefahamisha kwamba maeneo yeye matatizo hayo kwa Tanzania yamekuwa na malalamiko makubwa miongoni mwa wananchi jambo abalo iwapo serikali haitochuka hatua za uhakika upo uwezekano wa kutoka madhara makubwa.
Amesema kwamba maeneo ya kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Mtwara ,Ruvuma , Nachingwea, Tunduru , Liwale na kwengineko kumekuwa kukishuhudiwa malalamiko makubwa kati ya wakulima na wafugaji pamoja na hifadhi za taifa kugombea mipaka huku kukiwa na malalimiko ya wafugaji kuporwa mifugo yao jamboa mbalo linaashiria kukosekana maeneowano miongoni mwa pande husika.
Amesema, chama hicho kinaitaka serikali kufuata mapendekezo ya kuundwa tume ya kushughulikia migogoro na malalamiko hayo kwa kuwa inaonekana kusambaa katika maeneo mbali mbali ya nchi ya Tanzania.