Beki na Nahodha Msaidizi wa Nigeria ‘Super Eagles’ William Troost-Ekong, ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika lililomalizika Jumapili (Februari 11), amesema angependelea kushinda taji hilo kuliko tuzo ya binafsi aliyopata kwenye michuano hiyo.

Ekong alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye michuano hiyo na jopo la CAF, ambalo liliangalia mchango wa kila mchezaji kwa timu yake, pamoja na mwenendo wao katika muda wote wa michuano hiyo.

Beki huyo amewashukuru Mashabiki wa Nigeria kwa sapoti yao na kuomba radhi kwa niaba ya timu hiyo kwa kushindwa kutwaa ubingwa, huku akiahidi Super Eagles watarejea wakiwa na nguvu zaidi baada ya kushindwa kwa mchezo wa mwisho.

Washindi wengine wa tuzo katika Michuano ya ‘AFCON 2023’ ni Mlinda lango wa Afrika Kusini Romwen Williams ambaye alimshinda Mlinga Lango wa Nigeria Stanley Nwabali na kuwa Kipa Bora wa Michuano hiyo.

Emilio Nsue wa Guinea ya Ikweta alishinda tuzo ya Ufungaji Bora baada ya kuwa kinara wa kupoachika mabao matano. Simon Adingra na Emerson Fae, wote wa Côte d’Ivoire, walishinda Mchezaji Bora Chipukizi na Kocha Bora.

Broos: Nilitamani kuacha kazi Bafana Bafana
Serikali inatambua mahitaji Vituo vya Afya - Dkt. Dugange