Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amesema Serikali inatambua mahitaji ya vituo vya afya katika kata za kimkakati ikiwemo Kata ya Utiri wilayani Mbinga na hivyo katika mwaka wa fedha 2024/25 inakusudia kutenga bajeti kwa kila jimbo nchini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya na kata hiyo itapewa kipaumbele.

Dkt. Dugange ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbinga Mjini (CCM), Jonas Mbunda aliyehoji ni lini serikali itapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya utiri iliyopo kwenye jimbo hilo.

Akijibu swali hilo, Dkt. Dugange amesema “Serikali inatambua mahitaji ya vituo vya afya katika kata za kimkakati ikiwemo Kata ya Utiri. Katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali inakusudia kutenga bajeti kwa kila jimbo kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya. Hivyo, Serikali itaipa kipaumbele Kata ya Utiri katika Jimbo la Mbinga Mjini.”

William Troost-Ekong aomba radhi Nigeria
NFF yamwita Paseiro mezani