Eva Godwin – Dodoma.

Takriban Watu 700 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa moyo kwenye kambi ya moyo ya Hospitali ya Benjamin Mkapa – BMH, iliyopo jijini Dodoma.

Daktari Bingwa Moyo wa BMH, Dkt Calvin Masava ameyasema hayo hii leo Februari 13, 2024 na kudai kuwa BMH inashirikiana na Madaktari sita kutoka Nchini Uholanzi kufanikisha kambi hiyo.

Amesema, “Lengo la kambi mbali na kutoa huduma lakini inalenga kubadilishana uzoefu na wenzetu kutoka Netherlands”

Dkt. Masava amefafanua kuwa, watakaokutwa na matatizo ya moyo watapatiwa matibabu katika Hospitali hiyo ya  BMH huku akiongeza kuwa, “hii ni kambi yetu ya kwanza ya pamoja na wenzetu kutoka nje kwa kwa mwaka huu.”

Serikali kuendeleza utafiti wa Maji ardhini
MAKALA: Wanyama 10 wenye akili zaidi Duniani