Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali inaendelea na zoezi la utafiti wa maji ardhini pamoja na uchimbaji wa visima 13, katika Jimbo la Buchosa lililopo Wilayani Sengerema.

Mahundi ameyasema hayo hii leo Februari 13, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Buchosa Eric Shigongo, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itakamilisha uchimbaji wa visima vya Maji, vilivyoanza kuchimbwa katika jimbo la Buchosa.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Mahundi amesema hadi sasa jumla ya visima sita vimechimbwa, ambapo kati ya hivyo vilivyopata maji ni visima vinne, vilivyochimbwa katika vijiji vya Bulolo, Nyonga, Bulyahilu na Izindabo.

“Kazi ya utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa visima inaendelea katika Vijiji vya Kisaba, Busikimbi, Kasalaji, Nyamiswi, Luharanyonga, Irenza na Bugoro ambapo unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni,”amesema Mahundi.

 

TAWTO yaunga juhudi za Polisi kupinga ukatili
700 kufanyiwa uchunguzi wa Moyo BMH