Mwanafunzi wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Lukobe Manispaa ya Morogoro,  Stephen Robert (16), amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandarua chumba kwake akidaiwa huenda hakupendezwa na kitendo cha kukemewa akihimizwa masomo.

Akizungunza baada ya kutokea tukio hilo baba mzazi wa Mtoto huyo anasema siku ya tukio February 21 alibaki nyumbani akidai anasumbuliwa na kichwa lakin ilipofika majira ya saa tisa alasiri akajinyonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo ambapo amesema chanzo cha tukio  Mtoto huyo alisemwa na wazazi wake kuwa abadili mwendendo wa maisha yake ya kuwa na tabia nzuri na kuhudhuria masomo shuleni jambo ambalo likamkera kisha kuingia ndani na kujinyonga

RPC Mkama amewataka watoto kufika katika Kituo cha polisi dawati la jinsia au Kwa viongozi wa mtaa Ili waeleze changamoto zao badala ya kuchukua maamuzi Magumu ya kujiua

Simba SC pumzi muhimu leo
Wapaza sauti Shule kukosa vyoo kwa miaka miwili