Mbali ya kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, Klabu ya Al-Itihad ya Saudi Arabia pia inadaiwa kuhitaji huduma ya Mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini, Son Heung-min dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Baadhi ya timu kutoka Saudia zilihitaji kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana ilishindikana, kufuatia Son mwenyewe kusema kwa sasa bado anahitaji kucheza soka la ushindani.

Al-Itihad inataka kuwasajili mastaa hawa wote wawili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji na kuna uwezekano pia Mshambuliaji wao tegemeo Karim Benzema akaondoka mwishoni wa msimu huu.

Hata hivyo, uwezekano wa Son kutua kwa wababe hao ni mdogo kwa sababu hana mpango wa kuondoka Barani Ulaya kwa sasa.

Mkataba wa Son unatarajiwa kumalizika mwaka 2025 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 23 za michuano yote na kufunga mabao 12.

Tanzania, Japan zajadili kuimarisha uhuiano
Azam FC yawekewa mtego Mbeya