Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu wanane kwa mahojiano kuhusiana na tukio la mauaji ya Farijara Hamis Mboya, maarufu kwa jina la Kotex (40), Askari Mgambo aliyekuwa akisimamia utozaji wa ushuru kituo cha bajaji Mbuyuni, Februari 21, 2024.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Simon Maigwa imesema tukio hilo lilitokea mtaa wa sokoni kata ya Bomambuzi na mwili wa Marehemu ulikutwa ukiwa na majeraha ya kupigwa na kitu butu kichwani na sehemu mbalimbali za mwili.

Amesema, kabla ya tukio hilo Marehemu alikuwa kwenye shughuli zake eneo la Mbuyuni na wakati akirejea nyumbani alishambuliwa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kumtuhumu kuwa ni mwizi.

Watuhumiwa hao, ambao majina yao yanahifadhiwa wanatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika, huku Polisi ikionya juu ya uchukuaji wa sheria mkononi kwamba ni kinyume cha sheria na wale wote atakaofanya hivyo hawatafumbiwa macho.

Polisi Manyara wazipa ahueni Kaya zenye mahitaji maalum
Tanzania, Japan zajadili kuimarisha uhuiano