Wananchi wametakiwa kujenga mazoea ya kulipa Kodi ya ardhi kwa hiari na kutambua kuwa suala hilo ni la lazima kwa maendeleo ya Nchi.

Mkuu wa Idara ya ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Magesa Magesa ameyasema hayo wakati akiongelea suala la migogoro ya ardhi na mwitikio wa ulipiaji ardhi katika Wilaya hiyo.

Amesema, “kwa mujibu wa sheria zetu za Tanzania tupo na ardhi za aina tatu ya kwanza ni ardhi ya Kijiji, ambayo utawala wake unafanyika chini ya sheria ya Ardhi no5 ya mwaka 1999 ardhi ya pili ni ardhi ya jumla ambayo ipo chini ya usimamizi wa Kamishna ambayo inasimamiwa na sheria ya ardhi no 4 ambayo inaitwa ardhi ya mjini na kwa ujumla inaitwa ardhi iliyotangazwa ama ardhi ya mipango miji.”

“Na ardhi ya tatu ni ardhi ya uhifadhi ambayo ipo katika sheria mbali mbali za uhifadhi kwa mfano sheria ya uhifadhi wa mabende, sheria za uhifadhi wa wanyama,ama za misitu, na kadhalika hivyo idara ya ardhi inasimamiwa sheria inayohusu ardhi,” amesema Magesa.

Aidha, amesema kuwa migogoro ya ardhi inaweza kutokea kutoka katika maeneo hayo yote lakini kwa mujibu wa sheria ya utatuzi katika Nchi hutumika katika mabaraza pamoja na Mahakama inayotumika katika Maswala ya Ardhi.

“Migogoro ya ardhi za mjini ina tokana na mtu na mtu lakini kuna migogoro inayotokana na mirathi ama ndoa na wakati mwingine huchangiwa na sehemu ya uyawala kwa maana ya watalaamu wa ardhi wenyewe ama Viongozi mbalimbali wanaohusika na maamuzi katika Maswala ya ardhi, alifafanua Magesa.

Jipya kuhusu mkanganyiko wa huduma za NHIF
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 3, 2024