Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya nishati ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya uchumi na maisha ya kila siku ya mwanadamu, hivyo ni lazima wanaoisimamia wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa uzalendo.

Rais Samia ametoa maagizo hayo kwa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO, pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), wakati wa hafla ya uapisho wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. James Peter Mataragio, lkulu Ndogo Tunguu mjini Zanzibar.

 

Aidha, Rais Sarnia ametaka kuwepo na mwendelezo wa utoaji wa taarifa wa mara kwa mara ndani ya Serikali na kwa umma iwapokuna matengenezo au hitilafu iii ijulikane na kuepusha manunguniko yanayosababishwa na kutokuwa na taarifa.

Kuhusu suala la Gesi Rais Samia ameitaka Wizara hiyo kuhakikisha inatengeneza mpango maalum wa usambazaji wa gesi iii iwe rahisi kualika sekta binafsi iweze kushirikiana nao na hivyo kufikia lengo tililokusudiwa la asilimia 85 ya kaya ziwe zinatumia nishati safi ifikapo mwaka 2031.

Benchikha: Hatutaidharau Tanzania Prisons
Ally Kamwe: Tunaitaka Asec Robo Fainali