Wizara ya masuala ya kigeni ya Nchini Urusi, imemuita Balozi wa Marekani Mjini Moscow, Lynne Tracy kumuonya na kumuelekeza kwamba itawaondoa Wanadiplomasia wote wa Marekani, iwapo taifa hilo halitoacha kuingilia mambo yake ya ndani.
Moscow, imetoa onyo hilo huku ikiwa inajiaanda na uchaguzi wake mkuu utakaoanza Machi 15 – 17, 2-024 ambao Rais Vladimir Putin ambaye tayari ameshaiongoza Urusi kwa miaka 20, ana uhakika wa kushinda tena.
Kupitia taarifa yake, Urusi imesema itaangaliahatua za kichokozi na kusambazwa kwa taarifa zinazohusiana na uchaguzi na operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine.

Nishati safi ya kupikia: Safari imeanza
Semfuko ataka umahiri kuakisi kasi ya uwekezeji