Serikali Nchini, imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa Wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote za kijamii.

Hayo yamebainishwa hii leo Machi 8, 2028 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kupitia uwakilishi wa Waziri wa Maendeleo ya jamii jJinsia, Wanawake na makundi maalum, Dorothy Gwajima kwenye viwanja vya shule ya Msingi Chinangali 11 Wilaya ya Chamwino, wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Dodoma.



Amesema, “katika kudhihirisha hili, Serikali imeendelea kuwezesha Wanawake kupitia Mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo, jumla ya Shilingi Bilioni 743.7 zimetolewa na kunufaisha watanzania 6,064,957, wakiwemo Wanawake 3,288,186 sawa na asilimia 54 na wanaume 3,556,359 sawa na asilimia 46.”

“Serikali itaendelea kuimarisha upatikanaji wa mikopo ili kuwawezesha Wanawake kupata mitaji ya biashara. Hii ni pamoja na kuimarisha mikopo isiyokua na riba ya asilimia 10 inayotolewa kwa makundi maalumu kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa,” amesema Majaliwa.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema Dodoma inafanya maadhimisho haya kila mwaka kwani mwaka 2023, yalifanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ambapo Wanawake zaidi ya 10,000 waliweza kushiriki.

“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi kwenye Mkoa wa Dodoma, na Mkoa wa Dodoma unaviongozi Wanawake kwenye kila nyanja kwa asilimia kubwa,” amesema.

“Hii inawapa shime Wanawake kugombea ngazi mbalimbali za uongozi Serikalini, na kwenye uchaguzi ujao tupige kura kwa wingi, wanawake jitokezeni katika kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi”. Amesem Senyamule

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yalianza mwaka 1911 kufuatia maandamano ya Wanawake wafanyakazi wa sekta ya Viwanda nchini Marekani, kupinga mazingira duni ya kazi kama vile ukosefu wa huduma za kijamii na uwepo wa vitendo vya unyanyasaji katika ajira.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 9, 2024
Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri