Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa Mwongozo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa lengo la kutoa maelekezo katika hatua za kufuata kwenye ufuatiliaji wa afua za maendeleo, hatua za kitaalamu za maandalizi ya viashiria vya utendaji wa taasisi, kuanisha utaratibu wa kusimamia takwimu zitokanazo na ufuatiliaji wa shughuli za taasisi na kutoa mwongozo wa maandalizi ya taarifa za ufuatiliaji, tathmini, utekelezaji na utendaji wa Serikali.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Anderson Mutatembwa wakati wa akifungua kikao kazi cha Kujenga Uelewa wa majukumu na Upimaji wa Utendaji wa Serikali ngazi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa jijini Dodoma.

Amesema mwongozo huo umewasilishwa katika ngazi ya Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi na Wasaidizi wa U&T ngazi ya Wizara, hivyo ni hatua muhimu katika kupata uelewa wa pamoja juu ya mwongozo husika na kutoa maoni kabla ya kusainiwa.

Mutatembwa ameongeza kuwa ,Mwongozo unaainisha muundo wa usimamizi na majukumu ya kila taasisi kwa ngazi za Kitaifa, Kisekta na Wizara, Idara zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo majukumu hayo yanaainisha kazi zinazotakiwa kutekelezwa, ili kukamilisha upimaji wa utendaji wa kila taasisi na kuwezesha upatikanaji wa taarifa za utekelezaji na utendaji wa kila siku au pindi zinapohitajika.

“Nisisitize tena, matumizi ya Mwongozo huu yatawezesha Serikali kufuatilia, kutathmini na kupima utendaji wa taasisi zote katika ngazi za kitaifa na kisekta na kujenga msingi wa uwajibikaji wa taasisi husika kwenye mchango wa maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi,” amesema Mutatembwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali, Sakina Mwinyimkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu amesema nivizuri kuwa na Muongozo huu ili kuweza kuwa na utendaji ulimzuri kwenye kazi kwa manufaa ya Serikali.

Akifunga kikao kazi hicho Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Wilson Mahela amewasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidi Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya tamthimini zenye uhalisia wa maeneo wanayofanyia kazi kwa lengo na kuinua Mapato ya maeneo yao na Nchi kwa ujumla.

 

Kamanda Jongo: Imam hajatekwa anashikiliwa kwa uhalifu
Kocha Asec awapeleka wananchi Nusu Fainali