Hughes Dugilo, Kibaha – Pwani.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo, ameagiza Bodi zinazowalilisha Serikali kwenye mashirika zenye hisa chache kusimamia kwa ukamilifu mashirika hayo kwa maslahi mapana ya Taifa.

Prof. Mkumbo ametoa maelekezo hayo Machi 15,2024 Kibaha Mkoani Pwani, alipokuwa akifunga kikao kazi cha siku tatu, kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na wajumbe wa Bodi na wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50.

Alisema kuwa yapo mambo ambayo serikali inawataka viongozi hao kuhakikisha wanayasimamia ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo akizungumza alipokuwa akifunga rasmi kikao kazi cha siku tatu kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na wajumbe wa Bodi na wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50, Kibaha, Mkoani Pwani.

Waziri huyo alieleza kuwa moja ya mambo ambayo Serikali inatamani kuona yanafanyika kwa Kampuni hizo, ni kuona zinawekeza nchini kwani zipo hapahapa.

“Mna nafasi ya kuhakikisha kwamba Makampuni haya yanawekeza Tanzania na kuendana na mazingira ya hapa nchini.

“Utakuta Kampuni kubwa Kutoka nje imewekeza nchini, lakini mazingira yao na namna wanavyoendesha Kampuni kama wapo kwao” amesema Prof. Mkumbo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida akitoa neno kwa wajumbe wa mkutano huo alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano huo.

Aliwataka viongozi hao kuwa na tabia njema na kuona ujuzi na mbinu ambazo zinazotumika kuhakikisha Kampuni zao zinafanikiwa.

Prof. Mkumbo amewataka viongozi hao kutoa mrejesho kwa Serikali ambayo wanaiwakilisha kwa tutoka taarifa za mambo mbalimbali katika makampuni yao.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchuchu, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi kuelezea kilichofanyika katika siku tatu za Mkutano huo Kibaha Mkoani Pwani.

“Serikali imeamua kuijenga na kuikuza Sekta binafsi katika nchi yetu ili itusaidie, na ukiangalia makampuni mnayofanyia kazi mengi ni Sekta Binafsi, hivyo kusimamia na kufanya kazi kwa weledi ili kuisaidia Serikali kufikia malengo yake” amesema Prof. Mkumbo.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Msajili wa Hazina, Amon Nnko, akiwasilisha maazimio ya Kikao hicho.

Ofisi ya Msajili wa Hazina iliwaketisha pamoja wajumbe wa Bodi na wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa chini ya asilimia 50 katika kiikao kazi cha siku tatu, Kibaha, Pwani kwa lengo la kuzungumza nao na kuwakumbusha matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kusimamia masilahi ya Taifa.

Chelsea yahofia kumkosa Victor Osimhen
Kamati yahimiza matumizi ya Gesi asilia Viwandani