Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imefanikiwa sana kuongeza ukaribu na wananchi kwa kusikiliza changamoto na kuzitatua kwa haraka kupitia Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR).

Mfumo wa SNR ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi pia ni kigezo cha utawala bora unaozingatia ushirikishwaji wa wananchi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 3 ya Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR), katika Viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja.

Amesema kitengo cha SNR kina wajibu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia njia mbalimbali kwa wananchi ili waweze kutumia vema Mfumo huu kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Rais Mwinyi amesema, katika kipindi cha Miaka 3 tangu kuanzishwa kwa Mfumo wa SNR jumla la malalamiko 13,517 yamepokelewa kati ya hayo 11,116 yamepatiwa ufumbuzi na 2,351 yanaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali.

Mabeyo: Magufuli aliniita, alijua hatapona
Wapeni kipaumbele Wakandarasi wazawa - Kamati