Serikali ya Sudan Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana kutokana na joto kali ambalo linaweza kuongezeka hadi 45C (113F).

Mamlaka ya Afya na Elimu ya Nchini humo, iliwataka wazazi kuwazuia watoto wao kucheza nje kwa muda mrefu, wakisema joto hilo linaweza kudumu kwa wiki mbili, huku ikiarifiwa kuwa kuna tarifa za vifo vinavyohusiana na joto kupita kiasi.

Kutokana na katazo hilo, Serikali imesema Shule yoyote itakayokaidi amri hiyo kuanzia Jumatatu ya leo Machi 18, 2024 itafutiwa usajili wake kwani wiki iliyopita, takriban watoto 15 waliripotiwa kufariki kutokana na homa ya uti wa mgongo na magonjwa mengine yanayohusiana na joto.

Imebainika: Komando alifanikisha kifo cha Rais
Mradi wa Maji Malungu kuwanufaisha maelfu Nyasa