Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini – TMA, imetoa angalizo kwa wakazi wanaoishi ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam, kwamba kuna uwezekano wa kukutana na hali mbaya ya hewa kwa siku tano na Mvua za siku tatu mfululizo.

Kupitia utabiri wake wa hali ya hewa, TMA imeeleza kuwa, maeneo mengine yanatakayokumbwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

 

TMA imeeleza kuwa, hali hiyo itakayosababisha mvua kubwa itaendelea hadi Machi 21, 2024 huku ikisema, “zingatieni na jiandaeni. Athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.”

Februari Mosi, 2024, TMA ilitoa utabiri wake ikieleza kwamba bado kuna viashiria vya mvua za El Nino hadi Aprili 2024, kwa maeneo yanayopata mvua kwa msimu mmoja.

Ulega: Horohoro kuchagiza shughuli ukuzaji wa uchumi
Halmashauri yapewa siku moja kuwasilisha madai dhidi ya MSD