Kwa mujibu wa Shirikiano la Kimataifa la Watafiti la Nature Human Behavior, wanadai kwamba kutabasamu kunaweza kufurahisha hisia za Mwanadamu na kuongeza ari ya mapigo ya moyo, utendaji na ufanisi wa kazi na kuruhusu mzunguko wa damu kufanya kazi yake vizuri na kuepuka magonjwa hasa yale ya afya ya akili.

Lakini hilo limeibua swali na kuwa sehemu ya mjadala wa muda mrefu kati ya watafiti wa Saikolojia kuhusu sura za uso iwapo huathiri uzoefu wa Binadamu kihisia, ambapo wazo linalojulikana kama nadharia ya maoni kupitia matokeo ya hivi karibuni yaliyochapishwa katika jarida la Nature Human Behavior, ulionesha jawabu la kushangaza.

Matokeo yalibainisha kwamba, jambo hilo halina nguvu ya kutosha kushinda kitu kama mfadhaiko, lakini inatoa maarifa muhimu kuhusu hisia za kutabasamu ni nini na zinatoka wapi na Wanasaikolojia bado hawana uhakika juu ya asili ya sehemu hii kuu ya hali ya mwanadamu inayoleta tabasamu.

Utafiti huo, uliongozwa na Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Stanford, Nicholas Coles na kwa pamoja walipata ushahidi dhabiti kwamba tabasamu kwa mwanadamu linaweza kumfanya awe na furaha zaidi na kuongeza siku za kuishi akisema Tabasamu la furaha linaweza kuwafanya watu wajisikie amani na uso wenye mikunjo unaweza kuwafanya watu wahisi hasira, kwahiyo uzoefu wa mhemko lazima uwe angalau kwa sehemu, kulingana na hisia za mwili.”

Hata hivyo, waliarifu kwamba Mwanamke wa kawaida hutabasamu takriban mara 62 kwa siku, wakati Mwanamume wa kawaida hutabasamu mara nane pekee kwa siku, ikimanisha kuwa Wanawake hutabasamu zaidi kuliko wanaume lakini hiyo hutokana na sababu ya muhimu zaidi kwamba jinsia hizo mbili zina utofauti wa misuli.

“Tunapata hisia mara nyingi na tunasahau au kushangaa jinsi uwezo huu ulivyo wa ajabu. Lakini bila mhemko, hakuna maumivu au raha, hakuna mateso au raha, na hakuna janga na utukufu katika hali ya mwanadamu, Lakini Utafiti huu unatupa jambo muhimu sana kuhusu jinsi uzoefu huu wa kihisia unavyofanya kazi,” alisema Coles.

Young Africans yaifungia kazi Mamelodi
Simba SC yatambia kambi ya Zanzibar