Wang’amuzi wa vipaji ‘MASKAUTl’ wa Real Madrid na Paris S-Germain walikuwepo Uwanjani mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa Kombe la FA kati ya Newcastle na Manchester City kumtazama kiungo kutoka nchini Brazil Bruno Guimarães Rodriguez Moura ambaye zimepanga kumsajili dirisha lijalo.

PSG na Madrid zimekuwa zikiwania huduma ya kiungo huyo wa Newcastle United kwa muda sasa, kutokana na kiwango ambacho amekionyesha.

Newcastle United imepanga kumuuza kiungo huyu mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili pesa zitakazopatikana zitumike kwenye kufanya usajili wa mastaa mbalimbali mwisho wa msimu huu.

Hii ni kwa sababu ipo kwenye hatari ya kupata rungu kutoka mamlaka za soka England kwa kukiuka sheria za matumizi ya pesa.

Bruno tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 40 za michuano yote na kufunga mabao matatu. Mkataba wa sasa wa Bruno unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

PSG pia inadaiwa kumfuatilia kwa karibu mchezaji mwingine wa Newcastle Alexander Isak mwenye umri wa miaka 24 na inataka kuimarisha kikosi chake ikiwa na ndoto ya kubeba Ligi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Benchikha afunguka kambi ya Zanzibar
Dkt. Mpango kumuwakilisha Rais Samia mkutano wa dharura SADC