Miezi michache iliyopita, Mgombea wa upinzani, Bassirou Diomaye Faye ambaye anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, alikuwa amekaa kwenye chumba cha gezera akiwa hafahamiki sana nje ya chama chake cha upinzani cha Pastef.

Sasa Faye anajiandaa kuwa Rais baada ya mpinzani wake mkuu kutoka Chama Tawala kukubali kushindwa, kufuatia uchaguzi uliofanyika siku chache tu baada ya Faye kuachiliwa huru.

Picha kubwa ya Bassirou Diomaye Faye wakati wa Kampeni.

Kiongozi wa chama chake mwenye umaarufu mkubwa, Ousmane Sonko ambaye alikuwa pia kizuizini alishitakiwa kwa uasi mwezi Julai na kuzuiwa kugombea katika uchaguzi, ili kumrithi Rais Macky Sall sasa anakuwa katika kiulizo cha Wananchi juu ya hatma yake.

Ousmane Sonko.

Umaarufu wa Sonko ndiyo umemsafishia njia kwa Faye ambaye hakuwahi kuwa kiongozi wa ngazi yoyote kisiasa mapaka kuibuka kutoka kivuli cha bosi wake wa zamani na hatimaye kutoka gerezani, kuchukua kijiti, siku yake ya kutimiza miaka 44 ya kuzaliwa na kuibuka mshindi.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza katika chaguzi 12 za urais zilizofanyika chini ya haki ya upigaji kura wa kidemokrasia tangu Senegal ilipopata uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka wa 1960 ambapo mgombea wa upinzani ameshinda katika duru ya kwanza ya upigaji kura.

Shambulizi la Moscow: Kwa mara ya kwanza Putin amekiri
Xavi aombwa kubaki FC Barcelona