Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta amesisitiza kwamba anataka Xavi Hernandez abaki kama kocha wa klabu hiyo baada ya msimu wa 2023/24.

Xavi alitangaza nia yake ya kuondoka Barca mwishoni mwa msimu wa 2023/24 miezi michache iliyopita kutokana na hali mbaya iliyowafanya kupoteza mechi mbili za EL Clasico na kujiondoa katika mbio za ubingwa wa La Liga. Tangu wakati huo, kiwango cha ‘La Blaugrana’ hao ndani kimeimarika sana.

Barca kwa sasa wamefurahia mechi 10 bila kufungwa katika mashindano yote, na hivi karibuni walijikatia tiketi ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 2020 kwa ushindi dhidi ya SSC Napoli.

Laporta amesema kuimarika kwa kiwango chake kumesababisha mashabiki kumtaka Xavi kubaki klabuni hapo, huku taarifa zikieleza kuwa kuna masharti matatu ambayo yakizingatiwa yanaweza kumfanya kocha huyo kubaki.

Moja ya masharti yaliyosemwa inaripotiwa kuwa Barca inamtaka Xavi haswa kubadili uamuzi wake, na akizungumza katika mahojiano na Mundo Deportivo, Laporta alitoa dalili kwamba hilo linaweza kutokea.

“Ndio, ndio, ndio, ndio, tayari anajua kwamba Barca wanataka Xavi abaki, lakini anatambua. Ningependa aendelee, lakini tayari nilimwambia wakati huo, aliposema juu ya shinikizo, kwamba hapa sisi huwa chini ya shinikizo na uzoefu ulio nao.

“Nilimuuliza kama kuna njia yoyote ya kubadilisha mawazo yake, lakini nilimuona akikabiliana na presha isiyoweza kushindikana ambayo inaweza kuonekana usoni mwake, nikamwambia atulie akiona hivyo.”

Sonko chanzo Faye kuokota Dodo chini ya Mwarobaini
MALIMWENGU: Changamoto ni kama Ndimu kwenye Supu