Klabu Bingwa nchini Hispania FC Barcelona imesema inatarajia kumuuza mchezaji wake Ansu Fati mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anayekipiga kwa mkopo katika timu ya Brighton ya nchini England, atauzwa mwishoni mwa msimu huu kwenda timu watakayofikia mwafaka.

Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu ya Barcelona, ilisema kuwa wanatarajia kumuuza mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa hiyo ilisema watamuuza Ansu Fati baada ya baadhi ya timu kuonyesha nia ya kuitaka saini yake.

Imeeongeza kuwa, waliamua kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo kwenda Brighton kuhakikisha anaongeza kiwango chake tangu mwaka jana.

“Tulimtoa fati kwa mkopo kwenda Brighton lakini ameshindwa kupanda kiwango, hivyo tumefikia mwafaka wa kumuuza mwishoni mwa msimu huu,” ilisema taarifa hiyo.

Fati amecheza mechi 15 katika kikosi cha Brighton na kufanikiwa kufunga mabao mawili pekee.

Kocha Taifa Stars hajaridhishwa